HUDUMA ZA KOMPYUTA

HIZI NI MIONGONI MWA HUDUMA ZETU NA MAELEZO

Utangulizi
Ni jambo lililo wazi katika jamii yetu ya kwamba kuna wengi ambao humiliki Kompyuta au simu zenye uwezo wa juu,hali ya kuwa elimu ya kuvitumia vifaa hivyo ni ndogo kwao.Hii kutokana na kuwa,mambo mengi yanayohusiana na uendeshaji wa kimaisha ikiwemo utafutaji wa elimu na masuala mengi ya kibishara yamewekwa katika mfumo wa kidijitali,,mfumo ambao msingi wake ni matumizi ya Kompyuta.
Hivyo ,wengi hujikuta wakilazimika kutumia kompyuta au simu zenye uwezo mkubwa kabla hata ya kujiunga na kozi maalum zinazo husiana na matumizi ya vifaa husika.
Hali hii imetupelekea kuzitangaza huduma zetu katika lugha yetu ya Taifa (kiswahili).Richa ya matumizi ya lugha hii,katika matangazo yetu,baadhi ya maneno tumeyatohoa kama yalivyo kutoka katika lugha yake ya asili,hali ambayo  imepelekea baadhi ya huduma kuendelea kutoeleweka kwa urahisi kama ilivyo kuwa katika lugha yake ya asili.
 Kutokana na hali hii,tumeamua kuchukua hatua za makusudi kuzirudia kuziorodhesha huduma zetu,kama zilivyoorodheshwa katika ukurasa wetu wa awali (Home) zikifuatiwa na maelezo au ufafanuzi juu ya huduma hizo.Kumbuka BTC tunakupenda na tunakutakia mafanikio katika kila huduma unayofanya hasa inayojumuisha matumizi ya zana za kijitali.

HUDUMA ZETU
Tunaweka windows,katika Kompyuta zilizo na zisizo na milango ya CD {CD-ROM}.

WINDOWS   ,ni kifupi cha Microsoft Windows.Ni softiwea kuu iliyotengezwa kuziendesha program za hiari na zisizo za hiari katika kompyuta huku ikimrahisishia mtumiaji wa kompyuta husika kuzitumia program za hiari kupitia nyezo ya mfumo wa uwakilishi unaotumia alama za pekee za picha kuziwakilisha program hizo.
 Mfumo mkuu wa kisoftiwea unaoendesha shughuli zote za kompyuta huitwa Oparating system(O.S). Bila mfumo huu katika kompyuta,hakuna kitakacho weza kufanyika kupitia kompyuta hiyo.
Windows ni miongoni mwa Oparating system.Oparatimg system aina za Windows zimetengenezwa,na kuingizwa sokoni na kampuni inayojulikana kwa jina la Microsoft.
Windows ni jina la familia lililo kusunya operating system nyingi zinazofanya kazi kwa kutumia mfumo huo (wa windows).Miongoni mwa operating system aina za windows ni : Windows XP,Windows 7,Windows 8.1 na Windows 8.1 mobile.





Windows hupatikana dukani kupitia CD na DVD maalum,ambamo ndani ya makasha yake, mteja amepewa maelezo yanayohusiana na windows husika ,ikiwemo na maneno/namba za siri za pekee zinazoifanya windows hiyo kutamburika kuwa ni halisia kutoka kwa watengenezaji.
Mtumiaji wa kompyuta anapoweka windows katika kompyuta yake  bila maneno/namba za siri,hupewa nafasi ya siku 30 ambazo ni sawa na mwezi mmoja kuitumia kompyuta yake.Baada ya hapo atatakiwa kuweka windows nyingine au kununua namba za siri kutika kwa mawakala wauzaji wa bidhaa za Microsoft .
Ili kumuuepusha mtumiaji wa kompyuta na usumbufu na kupoteza gharama nyingi za kununua CD au DVD za windows,BTC tumechukua hatuastahiki ya kumhudumia mtumiaji huyu kwa kumuwekea Windows aitakayo,katika kiwango cha ubora,na katika gharama asiyoitegemea.

Kwa mahitaji ya Windows,karibu BTC-Computer Solution ,tukuhudumie.