Watambue Virus

VIRUS ZA KOMPYUTA NA ATHARI ZAKE.
VIRUSI NINI?
Ni programu haramu yenye uwezo wa kujisambaa ndani ya kompyuta na kujiingiza ndani ya programu halali zinazotakiwa kufanya kazi mle.
Ikisambaa inaathiri programu halali na kusababisha hasara/madhala makubwa.
VIRUSI ZINASAMBAA KWA NJIA YA;
1.      INTERNET
2.      CD/DVD
3.      FLASH DISKI
4.      MEMORY CARD
5.      KUDOWNLOAD PROGRAM ZISIZOELEWEKA/MANUFAA
ATHALI ZA VIRUS / MADHARA YATOKANAYO NA VIRUS;
1.      Virusi wanaweza kuharibu mafaili ktk kompyuta na kuyafanya shortcut
2.      Kupunguza uwezo wa ufanyaji kazi kwa kompyuta yako (computer very slow).
3.      Virus wanaweza kukuibia taarifa zako binafsi, na kugushi document zako na kukuletea matapeli wa mitandao na ukajikuta umepata fedheha kubwa.
4.      Kompyuta yenye virusi huwa inachelewa kuwaka.
5.      Mara nyingine hujizima na kujiwasha (RESTART)
6.      Kompyuta yenye virusi pia huwa mara nyingine inajizima kabisa na hata ukibonyeza kitufe cha kuwashia huwa haiwaki tena.
7.      Mara nyingine kompyuta yenye virusi huwa inatengeneza mafaili ya ajabu ajabu bila wewe kujua.
8.      Na mafaili hayo huifanya kompyuta yako ionekane kama vile hard disk yake imejaa wakati hujaweka chochote cha maana.