ELIMIKA NA TEHAMA

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------
[   IJUE TEHAMA ][  KISWAHILI NA TEHAMA ] 
___________________________________________________________________________________

IJUE TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO


( INFORMATION TECHNOLOGY )


 MAANA YA TEKNOLOJIA

Teknolojia ni elimu inayohusu uhandisi, ufundi, ujenzi ,vifaa na mbinu za uzalishaji wa vifaa na huduma katika jamii.

Pia tunaweza kuielezea Teknolojia kama ifuatavyo.
Teknolojia ni mabadiliko ya kisayansi yaliyowekwa kwenye nadharia ya utendaji kazi. Mabadiliko hayo yanapochochewa kwa kiasi kikubwa huwezesha mambo mbalimbali kuvumbuliwa na kuweza kuboresha shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na hata mawasiliano.

Neno “teknolojia” limetokana na neno la   
Kigiriki "τέχνη" (tamka: tékhne): likiwa na maana „uwezo, usanii, ufundi".
Teknolojia inaweza kumaanisha :
o   vifaa na mashine zinazotumika katika matengenezo au uzalishaji wa vitu
o   elimu ya matumizi yake pamoja na mbinu na maarifa jinsi ya kutumia sayansi.
o   uwezo wa kubadili malighafi asilia na kuwa bidhaa yenye thamani inayoweza kukidhi mahitaji ya binaadamu. Hapa bidhaa haimaanishi tu vitu kama magodoro, magari ya kutembelea,unga wa ngano n.k, la hasha ni huduma yeyote inayotolewa kwa jamii mfano huduma ya usafiri, huduma ya utalii, huduma ya chakula, na pamoja na vitu vyote vinavyozalishwa viwandani.

Asili ya teknolojia ni historia ya ubunifu wa vifaa na mbinu za kutumia vifaa hivi katika uzalishaji wa mahitaji, bidhaa na huduma katika jamii.

 KOMPYUTA


Unaelewa nini kuhusu kompyuta?

Kompyuta ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wa kupokea na kuhifadhi taarifa (Data), kufanyia kazi na kutoa matokea ya kazi hiyo na namna ilivyoendeshwa, pamoja na kutoa matokeo ya kitu kilichofanyika, yaani kinachoonekana (Information).

Pia unaweza kuitafsiri kompyuta kama ifuatavyo.
Kompyuta ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wa kuhifadhi taarifa(data), kupokea, kuendesha na kuzifanyia kazi taarifa(data) na kutoa matokea ya kazi iliyofanyika juu ya taarifa(data).
Kompyuta ni moja kati ya nyenzo zilizotokana na mabadiliko ya teknolojia ya hali ya juu



HISTORIA YA KOMPYUTA

HATUA KABLA YA MWANZO WA KOMPYUTA (1642)

Msomi mmoja kutoka Ufaransa aliyekuwa anaitwa Pascal, alianzisha chombo cha kufanyia hesabu, ambacho alikitengeneza kwa ajili ya kumsaidia baba yake katika kazi za hesabu, lakini hakikuwa na sifa bora kama ilivyotakiwa. Kisha baada ya hapo kiliendelezwa na msomi mwengine kutoka Ujerumani, ambaye alijulikana kwa jina la Lebnitz na kuzidishwa ubora zaidi, kikawa kinafanya kazi zote za hesabu, kama vile kujumlisha, kutoa, kugawanya na kuzidisha, badala ya kufanya kazi za kuzidisha na kugawanya tu. Kisha msomi mwengine kutoka Uingereza alikuja kuanzisha chombo chengine cha hesabu, ambacho kilikuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu. Chombo hicho kilikuwa na sehemu kuu tatu, ambazo sehemu ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kuhifadhia kumbukumbu, sehemu ya pili ilikuwa ni kwa ajili ya kufanyia hesabu,na sehemu ya tatu na ya mwisho ilikuwa ni kwa ajili ya kuchapishia.


HATUA YA MWANZO (1944)

Kipindi cha mwaka 1944 kinajulikana kuwa ni mwanzo wa kudhihiri kompyuta. Kompyuta katika kipindi hicho ilikuwa ina sura tofauti na hivi sasa, kwani ilikuwa ni kubwa mfano wa chumba, na ilikuwa inatumika kwa ajili ya kufanyia hesabu tu, na ilikuwa inajulikana kwa jina la ENIAC( Electronic Numerical and Calculation). Na mwisho wa mwaka 1951 kulianzishwa kompyuta nyingine ambayo ilikuwa inaitwa Unifac, na ilitengenezwa kwa ajili ya kufanyia biashara, na ilikuwa ni chombo pekee ambacho kilikuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu.



 HATUA YA PILI(1958)


Kipindi cha mwaka 1958 kilifanikiwa kuendeleza chombo cha kompyuta,ambapo kulianzish
 wa chombo kilicho julikana kwa jina la Transistor ambacho kiliwezesha kutengeneza kompyuta yenye umbo dogo baada ya kuwa na umbo kubwa mfano wa chumba. Vile vile chombo cha Transistor kiliwasaidia watumiaji wa kompyuta kipindi hicho kuepukana na joto kali lililokuwa linatoka kwenye kompyuta hiyo na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.Na mwanzo wa miaka ya sitini shirika la IBM lilianzisha chombo chengine cha kompyuta ambacho kilikuwa na maendeleo zaidi katika kipindi hicho






























HATUA YA TATU (1964)

Kipindi hichi kilileta maendeleo makubwa sana katika kompyuta, ambapo chombo cha kompyuta kilitengenezwa kwa kutumia (Integrated Circuits) chombo hicho kilichukua nafasi ya Transistor. Na pamoja na maendeleo makubwa kutokea mwaka 1972 shirika la Intel lilifanikiwa kutengeneza Processor ndogo ambayo ilibadilisha sura nzima ya kompyuta katika umbo dogo sana (Mini Computer). Na hiyo ilikuwa ni sifa pekee ya mabadiliko makubwa ya kompyuta, na katika kipindi cha mwaka 1975 shirika la IBM lilianzisha kompyuta ya kutumia mtu mmoja (Personal Computer), vile vile katika kipindi hicho zilianzishwa program za kuendeshea vifaa vya kompyuta, na miongoni mwa program hizo ilikuwepo program ya (Dos) Disk Operating System, Application Programs, na program za kutengeneza picha (Graphics).

HATUA YA NNE (1982)

Mwanzoni mwa miaka ya themanini kulianza kuenea matumizi ya kompyuta zenye kutumia Hard disk, na Processor zenye umbo dogo (Micro Processors) pamoja na program za kuendeshea kompyuta (Operating System). Pia zilianzishwa kopi za program za kuendeshea kompyuta (Dos), na hapo ndipo ilikuwa mwanzo wa kutumia Operating System aina ya Windows, na pia zilitumika program nyingine ndani ya Windows kama vile Word, Word 2, Word 6, Excel na power Point.
 

HATUA BAADA YA HATUA YA NNE (1995)

Kitu kinachosifika sana katika kipindi hichi ni kudhihiri kwa Operating System za Windows na kuwa kama ni mazingira pekee ya kuendeshea kompyuta, na inajulikana wazi kwamba windows ni kiini cha uendeshaji katika kazi za kompyuta, na imeitwa windows kwa sababu unaweza kuitumia kufanyia kazi nyingi kwa wakati mmoja kwenye madilisha tofauti, kwa mfano pale mtumiaji anapokuwa anasubiri window moja ifunguke anaweza kuwa anasoma au kufanya kazi nyingine kwenye window nyingine pia. Na windows ya kwanza kudhihiri ilikuwa ni Windows 95, 98, 2000, Millennium kisha Windows XP, vili vile zilianzishwa program maalumu kutoka kwenye shirika la Microsoft, kama vile Microsoft Office 97, Microsoft Office 2000 na Microsoft Office 2003,ambazo zinakusanya ndani yake Microsoft Word, Excel, Access na Power Point, pia zinajulikana kwa jina la application programs. Kisha kiliendelezwa kifaa cha Processor kutoka Pentium kwenda Pentium 2, Pentium 3 na Pentium 4. Wakati huo pia, ilizidishwa nafasi ya kuhifadhia data ndani ya Hard disk kiasi cha kufikia Giga Byte (GB) 300, na kufikia nafasi ya Ram zaidi ya Mega Byte (MB) 512.


MATUMIZI YA KOMPYUTA


Elimu

Kutokana na kuendelea kwa elimu ya teknolojia imetusaidia sana kujifunza mambo mbali mbali kupitia kompyuta, ambapo unaweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kuuliza maswali na kujibiwa kwa haraka tena kwa njia tofauti, pia unaweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kielimu, pia unaweza kuandaa vipindi mbalimbali vya masomo darasani. Pia unaweza kuoneshea filamu za maigizo zenye maadili,pia mandhari zenye kuelimisha kama vile mandhari za kijeografia na ugunduzi wa kisayansi.


Mawasiliano

Kompyuta inaweza kutumika kwa mawasiliano iwapo itaunganishwa na kompyuta zingine kwenye network au enternet.Watu wanaweza kuwasiliana kwa maandishi,sauti au au sauti na picha(video chat). 


Usafirishaji

Kompyuta pia hutumika kuongozea shughuli za usafirishaji zikiwemo za ardhini (mabasi, metro na treni),  majini (meli), na angani (ndege).


Viwandani

Kompyuta  hutumika viwandani kuendeshea mitambo ya uzalishaji, kama vile uzalishaji wa silaha za kivita, magari na vyakula katika viwanda husika.Teknolojia hii hutumika kwa kiasi kikubwa katika nchi zilizo endelea na zinazoendelea.



Ujenzi

Kompyuta hutumika kuandalia ramani za ujenzi wa majengo , miundo mbinu ya usafirishaji pamoja na mipango miji.

Matibabu 

Kompyuta pia hutumika katika shughuli za kimaabara (uchunguzi) na matibabu hospitalini.Kompyuta kupitia program maalum inaweza kugundua matatizo yaliyopo ndani ya mwili wa mgonjwa ,pia inaweza kupendekeza hatua za kufuatawa kuondoa tatizo. Kwa mfano; Kompyuta inaweza kumchagulia miwani mgonjwa wa macho yenye lenzi inayo endana na macho yake.


Burudani
Kupitia kompyuta mtumiaji anaweza kuburudika kwa kuangalia filamu azipendazo, pia anaweza kucheza gem kupitia program husika.,kama vile gem za mashindano ya magari au mpira.
  ________________________________________________________________________________
[   IJUE TEHAMA ][  KISWAHILI NA TEHAMA
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------